Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuwatia mbaroni jumla ya watuhumiwa 130 katika mikoa mbalimbali kwa tuhuma za kupanga na kuhamasisha vitendo vya kihalifu nchini ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kutumia vikao vya ndani na mitandao ya kijamii kuratibu mikakati ya kuvuruga amani na usalama wa taifa kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu.
Akizungumza kuhusu uzito wa njama hizo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, amefichua mipango ya hatari iliyokuwa imeandaliwa na wahalifu hao akisema kuwa vitendo hivyo vya kihalifu vilikuwa ni pamoja na kupanga, kutamka, kuandaa na kusambaza taarifa za uchochezi, kuhamasisha watu kushiriki katika vitendo vya kihalifu vikiwepo kuua baadhi ya viongozi na wananchi.
"Walikuwa pia wamepanga na kuratibu kuchoma shule mbalimbali, kulipua transforma za umeme ili nchi iwe gizani, kuharibu na kupora mali za umma na za watu binafsi sambamba na kuua askari wa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupora silaha.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment