NDARO, TX DULLAH, KIDEGE NA AZABOI WAWABURUDISHA MAFUNDI SHINYANGA
Wasanii wa vichekesho Ndaro, TX Dullah, Kidege na Azaboi wamewapa burudani washiriki wa semina ya mafundi iliyoandaliwa na kampuni ya MAGIC BUILDERS katika Ukumbi wa Lyakale, Manispaa ya Shinyanga.
Kupitia maonyesho yao ya ucheshi, wasanii hao waliibua vicheko na shangwe miongoni mwa washiriki, huku wakitumia sanaa yao kuhamasisha umuhimu wa umoja, amani, bidii katika kazi na maadili mema katika jamii.
Washiriki wa semina hiyo walionekana kufurahia burudani hiyo, wakisema imeongeza hamasa na kufanya mafunzo hayo kuwa ya kuvutia zaidi. Burudani hiyo ilikuwa sehemu ya kuhitimisha semina iliyolenga kuwajengea uwezo mafundi pamoja na kuhamasisha uzingatiaji wa taaluma, haki na wajibu wao katika sekta ya ujenzi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment