Na Mapuli Kitina Misalaba
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kulinda na kudumisha amani, akisisitiza kuwa usalama ni jukumu la kila mwananchi.
Amesema kila mtu ana haki ya kufanya kazi, kuendesha
biashara na kutekeleza shughuli zake za kila siku katika mazingira ya utulivu
na usalama, hivyo ni muhimu kuepuka vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.
Kuhusu masuala ya maandamano, Kamanda Magomi amesema
shughuli hizo zinapaswa kufanyika kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za
nchi, huku akiwataka wananchi kutoshiriki vitendo vya uchochezi au uvunjifu wa
sheria vinavyoweza kuhatarisha usalama wa watu na mali zao.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kusimamia
utekelezaji wa sheria kwa haki na weledi ili kuhakikisha Mkoa wa Shinyanga
unaendelea kuwa salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo
bila hofu.
Baadhi ya mafundi walioshiriki semina hiyo wameahidi
kuendelea kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na kuzingatia maadili ya taaluma
huku wakilinda amani ambayo ndiyo msingi wa maendeleo ya sekta ya ujenzi na
Taifa kwa ujumla.
Semina hiyo ilihitimishwa kwa burudani kutoka kwa
wasanii mbalimbali wakiwemo mchekeshaji Ndaro, pamoja na TX Dullah, Kidege na
Azaboi, ambao wametoa burudani iliyowavutia washiriki wa semina hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, akizungumza na mafundi katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya MAGIC BUILDERS mjini Shinyanga
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Patrobas Katambi, akizungumza na mafundi katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya MAGIC BUILDERS mjini Shinyanga
Mkurugenzi wa kampuni ya MAGIC BUILDERS, David Barongo, akieleza dhamira ya kampuni hiyo ya kuwawezesha mafundi kupitia mafunzo ya kuongeza ujuzi, kuwarasimisha na kuwapatia vyeti vya taaluma kwa kushirikiana na Serikali pamoja na Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Shinyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, akitoa elimu kwa washiriki wa semina kuhusu wajibu wa kila mwananchi katika kulinda amani, kuzingatia sheria na kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuhakikisha mazingira salama ya kazi na maendeleo yanaendelea kudumu.
Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali zilizolenga kuongeza ujuzi wa kazi, matumizi ya mikataba, uaminifu katika utekelezaji wa miradi pamoja na umuhimu wa kulinda amani kwa maendeleo ya sekta ya ujenzi.

Mamia ya mafundi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia kwa makini mafunzo yaliyotolewa katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya MAGIC BUILDERS, yenye lengo la kuwajengea uwezo, kuimarisha taaluma na kuhamasisha uzingatiaji wa sheria na maadili ya kazi.

Mmoja wa mafundi wenye bahati akikabidhiwa pikipiki kama zawadi maalumu kutoka kampuni ya MAGIC BUILDERS, ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi, kuwahamasisha mafundi na kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii na ubora.
Mmoja wa mafundi wenye bahati akikabidhiwa pikipiki kama zawadi maalumu kutoka kampuni ya MAGIC BUILDERS, ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi, kuwahamasisha mafundi na kuongeza ari ya kufanya kazi kwa bidii na ubora.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment