" MAPENDEKEZO 17 YAPITISHWA NA WADAU WA NGOs WILAYA YA KASULU KUIMARISHA MAENDELEO YA JAMII.

MAPENDEKEZO 17 YAPITISHWA NA WADAU WA NGOs WILAYA YA KASULU KUIMARISHA MAENDELEO YA JAMII.


Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) wamepitisha mapendekezo 17 yatakayosaidia kuimarisha uratibu, ushirikiano na ufanisi wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Kasulu kufuatia kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za mashirika hayo.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.Miongoni mwa mapendekezo yaliyopitishwa ni kuimarisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa miradi kwa wakati, kuongeza elimu kuhusu mikopo ya asilimia saba na asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri, kuimarisha ushirikiano kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za Serikali,kuhakikisha mashirika yanawasilisha taarifa zake kwa msajili kwa mujibu wa sheria.Mapendekezo mengine ni kuendelea kutekeleza shughuli za maendeleo zenye tija kwa jamii, kuboresha makundi ya WhatsApp kwa kuwaongeza wadau wapya wanaotaka kujiunga, wasajili kuweka wazi mashirika yasiyowasilisha taarifa kwa wakati na kuyawajibisha mashirika yanayoshindwa kuwasilisha taarifa kwa mujibu wa sheria n.kAkizungumza wakati wa ufunguzi wakikao hicho, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Isaac Anthony Mwakisu amewataka viongozi kuimarisha usimamizi  na kupokea ushauri kutoka kwa wataalamu na wenye uzoezi wa kuendesha mashirika ili yawe endelevu na yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii.Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Katibu Tawala wa Wilaya Theresia Mtewele amesema maoni na mapendekezo yaliyotolewa yafanyiwe kazi ili kuimarisha utendaji kazi wa mashirika yote na kuongeza mchango wake katika kuhudumia jamii.Kwa upande wao, wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) wamesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuimarisha ushirikiano na taasisi nyingine, kujifunza mbinu bora za utekelezaji wa shughuli na kubadilishana uzoefu unaochochea maendeleo ya mashirika yao.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


 

Post a Comment

Previous Post Next Post