Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Anthony Mwakisu ameambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye kuwatembelea na kuwapa pole wafanyabiashara walioathiriwa na ajali ya moto iliyoteketeza vibanda zaidi ya tisa nje kidogo ya soko katika Kata ya Muganza.Ajali hiyo imetokea Julai 10, 2026 huku chanzo chake kikitajwa kuwa ni mtu mmoja alikuwa akiandaa mafuta ya mawese kwa kuyapika ambaye aliwasha moto kisha akafunga mlango na kuondoka.Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Isaac Anthony Mwakisu amewataka wananchi kuzingatia kanuni na taratibu za ujenzi wa vibanda vya biashara kwa kuacha nafasi kati ya kibanda kimoja na kingine, kuhakikisha ufungaji wa umeme unafuata taratibu pamoja na kumtaka mtu aliyesababisha ajali hiyo kuripoti katika kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi.Aidha, Kanali Mwakisu amesisitiza umuhimu wa wafanyabiashara kuwa na vifaa vya kuzimia moto (fire extinguishers) katika maeneo yao ya biashara ili kupunguza madhara endapo ajali za moto zitatokea.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Mwl. Vumilia Julius Simbeye ameshauri kuzingatia matumizi ya vifaa vya ujenzi vilivyo imara ikiwemo kujenga kuta za matofali na kuepuka ujenzi wa kutumia mabanzi na nyasi ambavyo huongeza hatari ya kusambaa kwa moto.Vilevile, Mwl. Simbeye amelipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kushirikiana na wananchi katika kudhibiti moto huo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment