
Waandaaji wa Shinyanga Sukuma Festival and Business Expo Season 5 wametoa shukrani za dhati kwa wadhamini, washiriki, Serikali na wananchi wote waliochangia kufanikisha tamasha hilo lililofanyika mkoani Shinyanga.
Kupitia taarifa yao, wamewashukuru wadhamini wakuu na wateja kwa imani na ushirikiano wao, pamoja na washiriki wa maonesho ya biashara walioonesha bidhaa na huduma mbalimbali zilizochochea ukuaji wa biashara na uchumi.
Aidha, wamepongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa ushirikiano na usimamizi uliowezesha tamasha hilo kufanyika kwa mafanikio.
Waandaaji hao pia wamewashukuru vikundi vya sanaa, Kamati ya Maandalizi na wananchi wote kwa mshikamano na sapoti yao, huku wakiahidi kuendelea kuboresha tamasha hilo na kuwaletea wananchi matukio makubwa zaidi katika misimu ijayo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment