" MSD YAIBUKA KINARA KATIKA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST

MSD YAIBUKA KINARA KATIKA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST

 

Bohari ya Dawa (MSD) imeibuka kinara katika matumizi ya Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) baada ya kutunukiwa Tuzo ya Utendaji Bora katika Ununuzi wa Umma na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).

MSD imetambuliwa kama Taasisi Bora kwa Ujumla katika Matumizi ya Mfumo wa NeST kwa mwaka wa fedha 2025/2026, hatua inayoonyesha mafanikio yake katika kuimarisha uwazi, ufanisi na matumizi sahihi ya teknolojia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi wa umma.

Tuzo hiyo ilikabidhiwa Julai 29, 2026, wakati wa Kongamano la 10 la Kitaifa la Ununuzi wa Umma linaloendelea katika Ukumbi wa AICC, mkoani Arusha. Heshima hiyo inaendelea kuidhihirisha dhamira ya MSD ya kuzingatia misingi ya utawala bora na matumizi ya mifumo ya kidijitali katika kuboresha huduma za ununuzi wa umma.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post