Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi wa Kigoma baada ya kuzindua meli 4 za mizigo na kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho Mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma, baada ya kuwasili Katosho mkoani Kigoma, tarehe 20 Julai, 2026.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwahutubia wananchi wa Kigoma baada ya kuzindua meli 4 za mizigo na kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho Mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

Matukio mbalimbali katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka kumbukumbu ya Majina ya Wajenzi wa wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha Sita kutoka Tabora hadi Kigoma kwenye hafla iliyofanyika Katosho mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.

………… 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania ina nafasi kubwa ya kuwa kituo kikubwa cha biashara barani Afrika kutokana na rasilimali na fursa ilizonazo.

Ameyasema hayo Julai 20, 2026 mkoani Kigoma wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Tabora–Kigoma na uzinduzi wa meli nne za mizigo katika Bandari ya Kigoma.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora kisera na kisheria pamoja na kujenga miundombinu ya kimkakati ili kukuza biashara, uwekezaji, ajira na ustawi wa wananchi.

Amebainisha kuwa Kigoma haitabaki tena kuwa mwisho wa reli kama ilivyokuwa ikifahamika hapo awali, bali itakuwa mwanzo wa kufunguka kwa fursa za kibiashara na uwekezaji kutokana na miundombinu inayojengwa kuunganisha mkoa huo na masoko ya ndani na nje ya nchi.

Amesema mradi wa SGR Tabora–Kigoma wenye urefu wa takribani kilometa 506 unagharimu dola za Marekani bilioni 2.74, sawa na Shilingi trilioni 7.4, na utakapokamilika utaunganisha Kigoma na mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro hadi Dar es Salaam pamoja na mtandao wa reli unaoelekea Mwanza.

Aidha, amebainisha kuwa kukamilika kwa reli hiyo kutawezesha mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kufika Kigoma kwa haraka na kwa uhakika, jambo litakalopunguza muda na gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara na wajasiriamali.

Pia ameongeza kuwa SGR Tabora–Kigoma ni sehemu ya jitihada za kuimarisha nafasi ya Tanzania katika usafirishaji wa kikanda, huku Kigoma ikitarajiwa kunufaika kutokana na nafasi yake ya kimkakati inayoiunganisha Tanzania na nchi jirani.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254.