" RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) NA MELI NNE ZA MIZIGO MKOANI KIGOMA

RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR) NA MELI NNE ZA MIZIGO MKOANI KIGOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua miradi mikubwa ya maendeleo Mkoani Kigoma inayotarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuimarisha mzunguko wa biashara ndani na nje ya Mkoa huo.Hafla ya uzinduzi huo imefanyika katika eneo la Bandari ya nchi kavu Katosho lililopo Manispaa ya Kigoma Ujiji.Miradi hiyo ni ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma wenye urefu wa kilomita 506 unaogharimu shilingi trilioni 7.4 ambapo Rais Dkt. Samia ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo.Aidha, Rais Dkt. Samia amezindua rasmi meli nne za mizigo zitakazotoa huduma katika ukanda wa Ziwa Tanganyika hatua inayolenga kuimarisha usafiri wa majini  kuongeza ufanisi wa biashara na kuunganisha masoko ya Tanzania na nchi jirani.Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Balozi Simon Sirro amesema miradi hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za usafirishaji na kuufanya Mkoa wa Kigoma kuwa lango muhimu la biashara."Ujenzi wa reli hii utapunguza gharama za usafirishaji ambazo zilikuwa kero kubwa sana kwa wananchi lakini kwa  sasa mradi huu wa SGR utakuwa lango muhimu la biashara ndani na nje ya nchi, lakini pia tunaishukuru Serikali  kwa fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya hakika uchumi wetu utaenda kuwa mkubwa zaidi"Kwa upande wao, wananchi waliohudhuria hafla hiyo wameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa SGR na uzinduzi wa Meli za mizigo huku wakiahidi kuitumia kwa uangalifu pamoja na kuitunza.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post