Ni katika muendelezo wa ziara za mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, kusikiliza na kutatua kero za wananchi wilayani humo, ambapo leo amekutana na wananchi wa mtaa wa Mbulu, kata ya Mhongolo, Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule ya msingi Mbulu, Dc Nkinda amesisitiza uwajibikaji kwa viongozi na watendaji wa serikali, hususani katika kushughulikia changamoto za wananchi, badala ya kusubiri misafara ya viongozi wa kitaifa.
Katika mkutano huo, wananchi waliwasilisha kero zao, ikiwemo migogoro ya ardhi inayodaiwa kusababishwa na upimaji shirikishi wa viwanja, pamoja na madai ya ucheleweshaji wa utatuzi wa migogoro inayodumu kwa muda mrefu.
Aidha Nkinda amewataka wananchi kutoficha changamoto wanazokutana nazo, badala yake wazifikishe kwenye mamlaka husika mapema ili zipatiwe ufumbuzi.
"Msisubiri mpaka viongozi waje ndipo mseme, ofisi ya mkuu wa wilaya ipo, ofisi ya mkurugenzi ipo, viongozi wa kata na mtaa wapo kwa ajili ya kuwasikiliza na kutatua changamoto zenu, zileteni." Amesema Nkinda
Amewalekeza viongozi ngazi ya kata na mtaa kuitisha mikutano na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua, kwani wanao wajibu wa kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa haki, na kwamba kutoridhika kwa wananchi kunatokana na kushindwa kushughulikiwa kwa kero zao kwa wakati.
Awali baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mbulu walieleza kutoridhisha na shughuli ya upimaji shirikishi, walioeleza kuwa umewaongezea migogoro kwenye maeneo yao kuokana na kufanyika bila kufuata utaratibu.
Wananchi hao wameiomba Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko yanayohusu usimamizi wa upimaji wa ardhi na kuhakikisha migogoro hiyo inatatuliwa kwa haki.
Akijibu hoja hizo, Mpima Ardhi wa Manispaa ya Kahama Gennadio John amesema upimaji wa Mbulu ulifanywa kwa mfumo wa ushirikishwaji kupitia kampuni ya Geoplan, kwa kushirikiana na kamati za maeneo na wananchi.
“Kampuni iliyopewa dhamana ya upimaji ni maelekezo ya serikali. Lakini wananchi hawa wana changamoto ya maeneo yao kuingiliana. Tumeanza kutatua hizi kero kadri zinavyotufikia. Tumerejea upimaji.” Amesema John
Mwenyekiti wa mtaa wa Mbulu Mission Solomon Ruta amekiri kupokea maelekezo ya DC Nkinda huku akiahidi kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo.
“Kama wananchi walivyoto hoja mbalimbali, na wewe pia ukatoa maelekezo, nimeyapokea na nitayfanyia kazi tena kwa haraka sana.” Amesema Ruta
Mwisho.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment