
Rc Makalla asema ni fursa muhimu ya wananchi kufanya biashara,kujifunza na kuzijua teknolojia mpya za kilimo na ufugaji
Na Mwandishi Maalumu RS Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla ametoa wito kwa Viongozi, watendaji na wananchi wa Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi kwenye maonesho ya 32 ya Kilimo na mifugo na sherehe za nanenane, Kanda ya Kaskazini, zinazotarajiwa kuanza Agosti Mosi, 2026 kwenye Viwanja vya Themi Njiro Jijini Arusha kuanzia Agosti Mosi hadi 09, 2026.
Mhe. Makalla ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Maandalizi ya maonesho na sherehe hizo, ametoa wito huo leo Jumatatu Julai 27, 2026 alipoongoza kikao kazi cha Kamati hiyo, akisisitiza umuhimu wa kutofanya maonesho hayo kwa mazoea na badala yake yatumike kuongeza tija na kuimarisha shughuli za kilimo, uvuvi na ufugaji kwa wananchi.
“Sisi wenyewe Viongozi na watendaji tuwe mstari wa mbele kuhudhuria maonesho haya kwani ujio wetu utahamasisha pia wananchi wengine kuja kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo teknolojia mpya na uongezaji wa thamani wa bidhaa za kilimo, uvuvi na ufugaji.” Amesema Mhe. Makalla.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Hassan Babu ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa kamati hiyo amesisitiza umuhimu wa Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya kuhamasisha wananchi kuhudhuria maonesho hayo akimuhakikisha Mhe. Makalla kuwa Mkoa wa Kilimanjaro umejipanga vizuri kuhudhuria maonesho hayo kikamilifu.
Aidha Mwenyekiti Mwenza mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbeth Sendiga ameeleza kuhusu mpangilio wa wafanyabiashara katika maonesho hayo, akiitaka Kamati tendaji kuwapanga wafanyabiashara hao vizuri ili kuondoa msongamano wa watu katika baadhi ya maeneo machache ambao wengi wamekuwa wakifuata bidhaa fulani ambazo zimekuwa zikiwekwa eneo moja.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment