Mgodi wa Mwamba Mining uliopo Nyarugusu wilayani Geita mkoani hapo umepongeza hatua iliyofikiwa na wachimbaji wadogo katika eneo hilo kuondoka kwa hiari na kuwapisha wawekeze kwa teknolojia ya kisasa.Baadhi ya wachimbaji wadogo waliokuwa wanajihusisha na uchimbaji wa madini kwa kutumia lesseni ya Mwamba Mining wameondoka katika eneo hilo ili kupisha mwenye leseni kuendelea na shughuli zao za uchimbaji.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wachimbaji walikuwa katika eneo hilo wamepongeza Mgodi wa Mwamba mining kwa namna wa walivyokuwa na ukalimu wa kuwapatia muda wa kutosha takribani miezi mitatu kupisha eneo hilo.Mzee Juma shayo ambaye alikuwa ni mmoja wa wamiliki wa eneo hilo amepongeza uongozi wa Mwamba Mining ukiongozwa mkurugenzi wake pamoja na meneja wa mgodi huo Habil Ezekiel kwa namna ambavyo wamekuwa bega kwa bega na wenye maeneo hayo kuwapatia fidia ili waweze kupisha eneo hilo.Naye Pili Athumani ambaye alikuwa anajihusisha na uchimbaji katika eneo hilo amesema yeye akiwa mwanamke mwenye watoto sita aliyekimbiwa na mwanaume hivyo kwa kujishughulisha na uchimbaji kwenye mgodi wa Mwamba Mining anasomesha watoto wake na kajenga nyumba mbili.Meneja wa mgodi wa Mwamba mining kwenye eneo la Nyarugusu Habil Ezekiel ameshukuru sera za madini nchini kwa kuchochea ukuaji wa sekta hiyo huku zikiepusha migongano ya kijamii."Pamoja na kutokuwa tumeanza uchimbaji lakini tunashiriki katika huduma za kijamii kwa kusaidia watoto walio katika mazingira magumu" alisema Meneja.Ezekiel alisema kuwa mikataba ya uchimbaji madini imetoa mwongozo mzuri kwa wadau wote wanaotegemea eneo moja kuchimba madini wasiweze kuingia katika migongano.Alisema kumekuwepo upotoshaji juu ya wananchi waliopo kwenye eneo hilo kuwa walikuwa wanapinga kuwaachia eneo hilo kwa kusema si za kweli na zimelenga kujenga taswira hasi kwenye jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment