" WAFANYAKAZI WA TIANPIN INVESTMENT MANAGEMENT LTD WAMLILIA DC NKINDA, WADAI MAZINGIRA HATARISHI YA KAZI, UKOSEFU WA MIKATABA YA AJIRA

WAFANYAKAZI WA TIANPIN INVESTMENT MANAGEMENT LTD WAMLILIA DC NKINDA, WADAI MAZINGIRA HATARISHI YA KAZI, UKOSEFU WA MIKATABA YA AJIRA


Wamedai kukosa mikataba ya ajira, mazingira yasiyo salama, kutopatiwa vifaa kinga (PPE) pamoja na hofu ya kutoa malalamiko kutokana na kuogopa kufukuzwa kazi na mwekezaji wa kampuni hiyo mwenye asili ya China.

Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, wafanyakazi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikihatarisha usalama wao na afya zao wanapotekeleza majukumu katika shughuli za uchimbaji.

Meneja wa mgodi huo, Geofrey Msumali, amekiri kuwepo kwa changamoto hususani usalama na utoaji wa vifaa kinga kwa wafanyakazi, kutokuwa na mikataba huku akibainisha kuwa hata yeye hana mkataba wa ajira.

"Waliyosema ni kweli. Nadhani huyu mwekezaji haelewi kazi ya meneja, saivi wamenitenga, mambo yao hawanishirikishi, nikipeleka changamoto za wafanyakazi hazisikilizwi.”

Msimamizi mkuu wa mgodi huo Chen Faping amekanusha kuwepo kwa changamoto zilizolalamikiwa na wafanyakazi hao, akieleza kuwa vifaa kinga vipo na wanapewa, na mavazi ameagiza kutoka China baada ya siku 14 yatafika.

“Hakuna hiyo changamoto, vifaa kinga vipo stoo, mavazi tumeagiza baada ya siku 14 yatafika hapa. Naahidi.”

Mkuu wa wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, ameagiza kufanyika kwa uchunguzi na ukaguzi wa haraka ili kubaini ukweli wa madai yaliyotolewa na kuhakikisha sheria zinafuatwa.

Amesisitiza kuwa serikali inaita wawekezaji wengi lakini wafuate sheria, taratibu, na miongozo ya nchi inavyowataka badala ya kugeuka mwiba kwa wazawa wanaojitoa kufanya kazi kwenye kampuni hizo.

Amesema serikali itaendelea kusimamia usalama wa wafanyakazi na kuhakikisha waajiri wanazingatia sheria za kazi pamoja na kanuni za usalama migodini.

"Tutakwenda kukagua kama safety boots zipo. Kama hazipo kwa ajili ya wafanyakazi hawa, nnaelekeza wasifanye kazi kwenye mazingira hatarishi mpaka mtakapowapatia vifaa wanavyotakiwa kuwa navyo. Halafu anasema anasimamia stoo, kibali cha kutoka China kuja hapa ni kutunza stoo? Si hata mtanzania anafanya hiyo?”

“Naagiza watu wa mazingira kesho mapema wawepo hapa wafanye kazi yao ipasavyo, hii sio sawa kabisa na sisi kama serikali hatutakubali kuona hali kama hii.”

Mwisho.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post