" WAZEE DODOMA WATAKIWA KULINDA AMANI NA KUELIMISHA VIJANA

WAZEE DODOMA WATAKIWA KULINDA AMANI NA KUELIMISHA VIJANA

 

Wazee mkoani Dodoma wametakiwa kuisaidia serikali kwa kutumia hekima na busara zao kuelimisha vijana ili waendelee kuilinda amani iliyopo nchini bila kuangalia itikadi za vyama vyao. 

Kauli hiyo ilitolewa jijini hapa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Thomas Rutachunzibwa, alipokuwa akizungumza na wazee wa Kata ya Ipagala wakati wa chakula cha hisani kilichoambatana na ugawaji wa misaada iliyotolewa na Kanisa la Karmal Assemblies of God Tanzania (KAG) chini ya uongozi wa Askofu Mkuu Dk. Evance Chande. 

Dk. Rutachunzibwa aliwataka wazee hao kutumia nafasi zao kukemea watu wanaotaka kuvuruga nchi, akisisitiza kuwa wazee wana nafasi kubwa ya kushirikiana na serikali ili nchi iendelee kuwa na amani.

Kwa upande wake, Askofu Mkuu Chande aliwaomba Watanzania kuilinda na kuitetea amani ya nchi kwa njia zozote na kwa gharama yoyote kwa kuwa ikitoweka kuirudisha ni vigumu, huku akionya kuwa amani hiyo isipolindwa ipo hatari kubwa ya kuleta madhara kwa makundi yasiyojiweza wakiwemo wazee, watoto, wajawazito, na wenye ulemavu.

Alisema inasikitisha kusikia bado kuna baadhi ya Watanzania wanaoongozwa na watu wachache wasioithamini amani na wanaotaka kuvuruga nchi bila kujali madhara yanayoweza kuikumba jamii.

Katika hatua nyingine, akizungumza kwa niaba ya wazee wenzake wakati wa tukio hilo, mmoja wa wazee wa Ipagala, Ashura Kimwaga, aliainisha baadhi ya changamoto wanazokutana nazo ikiwemo ugumu wa kupata huduma katika maeneo muhimu kama vile kwenye sekta ya matibabu.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post