
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Zuhura Yunus, amewataka vijana hao kuonesha weledi na nidhamu waliyofunzwa nchini ili kuleta sifa zaidi kwa vijana na hivyo kuendelea kutanua soko la ajira kwa kuonesha weledi na uadilifu huko waendako.
Pamoja na hayo amesema mafunzo ya uzoefu wa kazi (Internship) na uanagenzi yanayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yameendelea kuwa msingi muhimu wa kuwaandaa vijana wenye ujuzi, umahiri na ushindani unaohitajika katika soko la ajira la ndani na la kimataifa.
Zuhura pia ametoa wito kwa waajiri wa sekta ya umma na binafsi kuendelea kutoa nafasi za mafunzo kwa vijana ili kuongeza idadi ya Watanzania wenye ujuzi wa vitendo na kuwajengea uwezo wa kunufaika na fursa zinazojitokeza duniani. Amesema uwekezaji katika maendeleo ya vijana ni hatua muhimu ya kuongeza tija ya Taifa na kufungua fursa zaidi za ajira kwa vizazi vijavyo.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi, Bi. Alana Nchimbi, amesema vijana hao wamepatiwa maandalizi muhimu kabla ya safari ikiwemo mafunzo ya kabla ya kuondoka nchini, elimu kuhusu haki na wajibu wao kazini, matumizi ya fedha, pamoja na elimu ya Hifadhi Scheme ya NSSF.
Amesema maandalizi hayo yanalenga kuwafanya kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa kuzingatia weledi, nidhamu na uadilifu wanapotekeleza majukumu yao nje ya nchi.
Katika hafla ya kuaga vijana hao Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala Binafsi wa Ajira (TRAA) Abdallah Mohamed amewasisitiza Vijana wanaoenda nje nchi kulinda tamaduni zao na kuheshimu tamaduni watakazo zikuta huko, kwani ndio sababu ya kuwafanya wao kuendelea kupata fursa zaidi huko ughaibuni.
Naye Meneja wa NSSF Wilaya ya Temeke - Juma Mwita,amesema mfuko huo utaendelea kulinda haki za wanachama wanaofanya kazi nje ya nchi kupitia huduma ya Hifadhi Scheme, inayowaruhusu kuendelea kuchangia mafao yao ya hifadhi ya jamii wakiwa ughaibuni, huku familia zao zikiendelea kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko kwa mujibu wa sheria.
Aidha , Meneja wa Diaspora Banking wa CRDB, Joseph Mosha, ameishukuru serikali kwa ushirikiano wake kupitia huduma ya Ughaibuni Loan, ambayo imewawezesha vijana wengi kumudu gharama za maandalizi ya safari za kwenda kufanya kazi nje ya nchi. Amesema benki hiyo itaendelea kutoa elimu na huduma za kifedha kwa Watanzania popote walipo duniani ili kuwawezesha kusimamia vizuri mapato yao na uwekezaji wao.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika, Jackline Adam ameishukuru Serikali kwa mafunzo na maandalizi waliyoyapata kabla ya safari, akiahidi kuwa yeye pamoja na wenzake watakuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na kuzingatia sheria za nchi wanazokwenda, huku wakitumia fursa hiyo kuboresha maisha yao, familia zao na kuchangia maendeleo ya Taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment