Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) wameendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watoa huduma za afya kuhusu uchukuaji wa sampuli za HPV na DNA kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake wenye umri wa miaka 30 hadi 65.Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Mji Kasulu na kuwashirikisha watoa huduma za afya kutoka Halmashauri ya Mji Kasulu na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.Washiriki wamepata maarifa na ujuzi utakaosaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi ambapo wawezeshaji walitumia mbinu shirikishi ikiwemo majadiliano, kuuliza maswali na kufanya mazoezi kwa vitendo jambo lililochangia kuongeza uelewa kuhusu uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kutumia kipimo cha HPV na DNA.Wawezeshaji wa mafunzo wakiwemo, Leonarda Muhchi, Novatus Nguse, Peter Mkama na Wambura Waryoba wamesisitiza umuhimu wa umakini na kuzingatia miongozo ya kitaalamu katika uchukuaji wa sampuli ili kuboresha ubora wa huduma za uchunguzi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya Wilayani Kasulu.Kwa upande wao, washiriki wameeleza kuridhishwa na mafunzo hayo wakibainisha kuwa yamewaongezea ujuzi na uwezo wa kitaalamu wa kuwabaini wanawake walio katika hatari ya kupata ugonjwa huo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254












Post a Comment