" MBINGA MJI KUJA NA MIKAKATI YA KUONGEZA MAPATO KUPITIA KAHAWA

MBINGA MJI KUJA NA MIKAKATI YA KUONGEZA MAPATO KUPITIA KAHAWA

 

Halmashauri ya Mji Mbinga imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wakulima, hususan wanaolima zao la kahawa, kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji na ukusanyaji wa mapato huku ikilenga kukusanya shilingi bilioni 5.7 katika mwaka wa fedha 2026/2027, huku zao la kahawa likitajwa kuwa miongoni mwa vyanzo muhimu vinavyoweza kuchangia kufikiwa kwa lengo hilo.

Akizungumza katika Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Mbinga, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Kisare Makori, amelitaka Baraza hilo kuweka mikakati madhubuti ya kutumia fursa inayotokana na zao la kahawa katika kuongeza uzalishaji wa zao hilo na mapato ya Halmashauri.

Makori amesema takwimu zinaonesha kuwa zao la kahawa limeendelea kuongeza mchango katika ukusanyaji wa mapato mwaka hadi mwaka, hivyo kuna umuhimu wa kuendelea kuboresha mazingira ya uzalishaji, uuzaji na usimamizi wa zao hilo.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Myangayanga, Norbeth Njako, amesema mafanikio yanayoendelea kupatikana katika zao la kahawa ni matokeo ya ushirikiano mzuri baina ya Idara ya Kilimo, AMCOS pamoja na vyama vya ushirika.

Amesema uimarishaji wa vyama hivyo umechangia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato kwa kudhibiti mianya ya utoroshaji wa kahawa, huku ukiwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji na hivyo kuongeza kipato chao pamoja na mapato ya Halmashauri.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya, Aureus Ngonyani, amesema Halmashauri tayari imejipanga kuandaa miche ya kahawa ya kutosha na kuwapatia wakulima kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

hatua hiyo itaongeza chachu ya kilimo cha kahawa na kuchangia kukuza uchumi wa wakulima pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post