" MWENGE WA UHURU WAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI USHETU, MITUNGI 50 YA GESI YAGAWIWA

MWENGE WA UHURU WAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI USHETU, MITUNGI 50 YA GESI YAGAWIWA


Mwenge wa Uhuru umeendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia katika Halmashauri ya Ushetu, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga, ambapo jumla ya mitungi 50 ya gesi imegawiwa kwa mama lishe, wakiwemo wanawake wenye ulemavu na wasio na ulemavu.Hatua hiyo inalenga kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati zinazochafua mazingira, hususan kuni na mkaa, na kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa ajili ya kulinda afya, mazingira na kupunguza gharama za uendeshaji wa shughuli za kila siku.Mmoja wa wanufaika, Eva Maziku kutoka Kata ya Kinamapula, amesema kupatiwa jiko la gesi kutamsaidia kupunguza gharama za kununua mkaa huku akilinda afya na mazingira.Amesema awali alikuwa akitumia hadi gunia moja la mkaa kwa wiki, ambalo katika eneo hilo hugharimu kati ya Shilingi 25,000 hadi 30,000.“Kwa kupata majiko haya, nitakuwa tayari nimetunza mazingira, na pia nitakuwa nimelinda afya yangu na kuokoa maisha yangu mimi kama mama. Ninamshukuru sana mama Samia kwa kutuona hata sisi akina mama lishe wa Ushetu, abarikiwe sana” Amesema MazikuKwa upande wake, Lucia Shija, mama lishe mwenye ulemavu wa viungo, amesema matumizi ya gesi yatamuepusha na changamoto ya kutafuta kuni porini, jambo ambalo kwake lilikuwa gumu kutokana na hali yake ya ulemavu.Amesema hatua hiyo pia itasaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni.Amesema “Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuona sisi wenye ulemavu, mimi nilikuwa natumia kuni kwa kukata kwenye mapori huko, na macho yanakuwa mekundu unaitwa mchawi, lakini sasa hivi nitapika vizuri.”Mratibu wa Nishati Safi wa Halmashauri ya Ushetu, Naomi Ndelwa, amesema Halmashauri hiyo imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika kata zote 20 na vijiji vyake kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia.Amesema hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safipikia kwa wananchi na kuendelea kulinda misitu na mapori ya akiba yaliyopo katika halmashauri hiyo.Amesema kati ya mitungi 50 iliyogawiwa, mitungi 25 imenunuliwa kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri, huku mitungi 30 ikitolewa na wadau wanaoshirikiana na Halmashauri katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.“Sisi kama Halmashauri tumejipanga kutoa elimu kwenye kata zote 20 na vijiji vyake, kuhusu umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa jamii nzima.” Amesem MbelwaKwa upande wake, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang’onda, amewataka wananchi kuendelea kulinda amani na utulivu nchini, akisisitiza kuwa mazingira ya amani ndiyo msingi wa kuendelea kupatikana kwa maendeleo.Amewataka wananchi kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, huku akisisitiza umuhimu wa watanzania kushirikiana katika kulinda amani na utulivu wa nchi.Amesema “Tulindeni amani na utulivu, nchi yetu iendelee kubaki na utulivu, tumuombee Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan nay eye ataendelea kutuletea maendeleo makubwa zaidi.”Mwisho

 

Post a Comment

Previous Post Next Post