
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Dkt. Joel Nanauka, amewataka vijana nchini kutambua mapema kusudi la kuwepo kwao duniani ili waweze kufanikiwa katika maeneo ambayo wengi wameshindwa.
Waziri Nanauka ametoa wito huo leo, Agosti 30, 2026, jijini Dodoma wakati akizungumza katika Ibada Maalumu ya Utamaduni iliyofanyika katika Kanisa la Destiny City.
Amesema siri ya kupiga hatua na kutofautiana na wengine walioshindwa inategemea zaidi uelewa wa kile ambacho mtu ameitwa na Mungu kukifanya duniani, badala ya kukimbizana na mambo bila kuwa na dira.
Mbali na hayo, Waziri Nanauka amewasihi waumini wa kanisa hilo na Watanzania kwa ujumla kudumisha uzalendo kwa kuipenda nchi yao na kuendelea kuiombea, ili Mwenyezi Mungu aendelee kulinda amani ya Taifa pamoja na viongozi wake.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment