" POLISI MWAMALILI WATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU

POLISI MWAMALILI WATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU

 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Sheila Zongo, amewataka wananchi wa Kata ya Mwamalili kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na vitendo vya uhalifu vinavyotokea kwenye maeneo yao.


​Rai hiyo imeitolewa wakati alipowatembelea wananchi waliokuwa wakipata huduma za afya katika Zahanati ya Kata ya Mwamalili, Manispaa ya Shinyanga

Mkaguzi Msaidizi Zongo, amewaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa za kuwepo kwa vitendo vya kihalifu, akibainisha kuwa mara nyingi wahalifu wanaojihusisha na matukio hayo wamo ndani ya jamii na familia zao.

​Aidha, ameeleza kwa kina lengo la mradi wa Jeshi la Polisi uitwao "FAMILIA YANGU HAINA MHALIFU", ambao unalenga kuelimisha na kuhamasisha kila familia kuwajibika kwa kuhakikisha haimfichi mhalifu yeyote.

Ushirikiano wenu wa kutoa taarifa za siri utasaidia kutokomeza uhalifu kabla haujaleta madhara makubwa kwenye jamii," alisisitiza Mkaguzi Msaidizi Zongo.

Post a Comment

Previous Post Next Post