Katika kuendeleza dhana ya Polisi Jamii na ulinzi shirikishi, Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Fraterine Tesha leo ametembelea na kukagua kampuni mbalimbali za ulinzi katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Akizungumza na viongozi wa makampuni hayo kwa nyakati tofauti alihimiza uhuishaji wa vibali vyote vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na vibali vya silaha ili kutoikosesha Serikali mapato yake na kuwataka kutoajiri watu ambao wanakosa sifa ikiwa ni pamoja na raia wa kigeni ama wale waliovuka umri wa miaka hamsini na tano ACP Tesha alipata nafasi ya kukagua silaha mbalimbali zinazotumika na kampuni hizo zikiwemo zilizokuwa katika malindo mbalimbali ndani ya Manispaa hiyo kwa lengo la kuzitambua na kuwahimiza askari hao kuzuia mihemko inayopelekea matumizi mabaya ya silaha kwani kila mmoja atawajibika mwenyewe mbele ya sheria kwa matumizi mabaya ya silaha.Sambamba na hayo aliwataka askari wa kampuni hizo kuwa waadilifu na kuzingatia usafi wakati wote kwa kuvaa sare kamili pamoja na filimbi wote wawapo katika majukumu yao.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment