NA MWANDISHI WETU MANYARA
Tarehe 09 September, 2026 imefunguliwa Kesi ya Uhujumu uchumi namba 20357/2026 mbele ya Mh. Erick Rwehumbiza Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya mbulu, dhidi ya Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. JUMA IBRAHIM MVUMI.
Mshtakiwa anashtakiwa kwa makosa sita (06) ya Matumizi mabaya ya Madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2019 ikisomwa pamoja na aya ya 21 Jedwali la kwanza na vifungu vya 57 (1) na 60 (2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi, pamoja na Makosa ya Kupangwa [Sura ya 200] marejeo ya 2019.
Mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Bw. Amiri Addy ameieleza mahakama kuwa Mtuhumiwa huyo alikiuka Kanuni za manunuzi pamoja na Miongozo ya FORCE ACCOUNT katika kufanya manunuzi ya Umma katika kutekeleza mradi wa "SUSTAINABLE RURAL WATER SUPPLY AND SANITAZATION PROGRAM (SRWSSP)" uliokuwa unatekelezwa katika halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kumpendelea mzabuni DOMA ENTERPRISES kwa kumpatia tender ya kusambaza vifaa vya ujenzi katika miradi hiyo yenye thamani ya Tsh. 31,217,920/= bila kushindanishwa.
Mshtakiwa amesomewa hati ya mashtaka na amekana mokosa yote sita (06) yanayomkabili.
Aidha, Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na Wadhamini wawili na Kudeposit nusu ya pesa ya thamani ya kesi ambayo ni Tsh. 15,000,000/= au kuwasilisha Hati ya Mali isiyohamishika iliyofanyiwa tathmini yenye thamani ya Tsh. 15,000,000/=, hivyo amepelekwa Mahabusu.
Shauri limehairishwa hadi tarehe 17.09.2026 kwaajili ya Hoja za awali (PH).
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment