Septemba 10, 2026 Mahakama ya Wilaya ya Mbulu Mbele ya Mh. VITUS KAPUGI, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya MBULU imetolewa hukumu katika shauri la Uhujumu Uchumi (Economic Case) namba 14623/2026 , dhidi ya Aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyamusta iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. DANIEL GIDAMBISYE MURAYDA pamoja na Mhasibu wa Shule hiyo Bw. JAMES COSMAS BAZIL.
Washtakiwa hao wanashtakiwa kwa makosa ya Matumizi Mabaya ya Madaraka kinyume na kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2022 ikisomwa pamoja na aya ya 21 Jedwali la kwanza na vifungu vya 57 (1) na 61 (2) ya Sheria ya Uhujumu Uchumi pamoja na Makosa ya Kupangwa [Sura ya 200] marejeo ya 2022.
Washtakiwa walifanya kosa hili kwa kukiuka kanuni za Manunuzi katika Manunuzi ya Umma katika kutekeleza Mradi wa WATER SANITAZATION PROJECT uliokuwa unatekelezwa katika shule ya Msingi Nyamusta katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kushindwa kushindanisha wazabuni na kutoa zabuni ya kusambaza vifaa yenye thamani ya TZS 26,447,217.10/= kwa upendeleo kinyume na Sheria, Kanuni za manunuzi ya Umma pamoja na Miongozo ya utekelezaji miradi kwa njia ya FORCE ACCOUNT
Washtakiwa wametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) gerezani au kila mmoja kulipa faini TZS 1,000,000/= (Milioni Moja)
Shauri hili lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa TAKUKURU Bw. Amiri Addy
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment