Mwenyekiti
wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia Sangalali,
amewataka wanafunzi, hususan wa kike, kusoma kwa bidii na kuweka elimu mbele
ili waweze kutimiza ndoto zao na kujenga maisha yao ya baadaye.
Chifu
Sangalali ametoa ujumbe huo wakati wa Tamasha la 19 la Himaya ya Jigoku,
Masela, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, akiwataka wanafunzi kutokukimbilia
kuolewa na kuacha masomo.
Amesema
elimu ni msingi muhimu wa maisha na amewataka wanafunzi kutumia fursa
wanazopata shuleni kwa kujituma katika masomo badala ya kuacha elimu kwa sababu
ya kuingia kwenye ndoa wakiwa bado katika hatua ya masomo.
“Nitumie
fursa hii kuwahimiza wanafunzi, hasa wa kike, someni sana, msikimbilie kuolewa
mkaacha masomo,”
amesema Chifu Sangalali.
Amesema
jamii ina wajibu wa kuwaunga mkono watoto katika safari yao ya elimu na
kuhakikisha wanapata mazingira yanayowawezesha kusoma na kutimiza malengo yao.
Ujumbe huo
umetolewa katika tamasha hilo lililolenga pia kuendeleza mila na tamaduni za
Kitanzania, kuimarisha mshikamano na kutoa elimu mbalimbali kwa jamii.
Chifu
Sangalali amesisitiza kuwa vijana wenye elimu wana nafasi kubwa ya kuchangia
maendeleo ya familia zao, jamii na taifa, hivyo amewataka wanafunzi kutumia
muda wao vizuri na kuweka juhudi katika masomo yao.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment