Mwenyekiti
wa Machifu Tanzania na Mtemi wa Himaya ya Jigoku, Chifu Antonia Sangalali,
amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza fedha za Tanzania kwa kuepuka
kuzichana, kuzitoboa au kuziandikia, akisisitiza kuwa noti hizo hutumika na
watu mbalimbali katika mzunguko wa fedha.
Chifu
Sangalali ametoa ujumbe huo wakati wa Tamasha la 19 la Himaya ya Jigoku,
Masela, Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, akisema amepokea ujumbe kutoka Benki Kuu
ya Tanzania na kuamua kuufikisha kwa wananchi kupitia nafasi yake kama
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania.
Amesema
wananchi wanapaswa kutambua kuwa noti wanazoshika leo zinaweza kutumika na mtu
mwingine kesho, hivyo ni muhimu kuzitunza ili ziendelee kuwa katika hali nzuri
na kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
“Benki
Kuu ya Tanzania ina ujumbe kwa Watanzania wote kupitia kwangu mimi nikiwa kama
Mwenyekiti wa Machifu Tanzania. Mzitunze pesa za Tanzania, msizichane,
msizitoboe, msiziandike,” amesema Chifu Sangalali.
Ameongeza
kuwa fedha ni mali inayozunguka katika jamii, hivyo kila mwananchi ana wajibu
wa kuhakikisha anaitunza kwa usalama na heshima.
Ujumbe huo
umetolewa sambamba na wito wa Chifu Sangalali kwa wananchi kuendelea kudumisha
amani, mshikamano na maadili, akisisitiza umuhimu wa kila mmoja kuwa na wajibu
wa kulinda ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Tamasha hilo
la 19 la Himaya ya Jigoku limewakutanisha ndugu wa utemi kutoka maeneo
mbalimbali nchini Tanzania pamoja na wageni kutoka Uganda, huku likinogeshwa na
burudani za ngoma za asili.
Mwenyekiti wa machifu Tanzania Mtemi Antonia Sangalali akishiriki kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa benki kuu ya Tanzania.
Picha ya pamoja.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment