NA, Egidia Vedasto, Misalaba Media, Arusha.
Mfumo wa e Audit Next Wajipanga Kuwanoa Wakaguzi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Saada Salum Mkuya, amewataka wakaguzi wa ndani wa Serikali na sekta binafsi kuwa na ujasiri na uhuru wa kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya fedha, hasa wanaposhiriki katika majadiliano yanayohusu matumizi na usimamizi wa rasilimali za umma.
Amesema wakaguzi wa ndani wana nafasi muhimu katika kuhakikisha rasilimali za fedha zinalindwa na kutumika kwa ufanisi, huku wakitoa ushauri unaolenga kuzuia upotevu na matumizi yasiyo sahihi ya fedha za umma.
Dkt. Mkuya amesema wakaguzi wanapaswa kutumia weledi, uadilifu na taaluma yao katika kutekeleza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto za kifedha na kutoa mapendekezo yanayoweza kusaidia taasisi kuboresha mifumo ya usimamizi na udhibiti wa fedha.
Amesema hayo Jijini Arusha wakati akizungumza katika Mkutano wa 19 wa Mwaka wa Ukaguzi wa Ndani na Mkutano wa 13 wa Mwaka wa Utawala Bora, ambapo amesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya ukaguzi na utawala bora katika kulinda rasilimali na kuongeza uwajibikaji katika taasisi.
Katika namna hiyohiyo Mkurugenzi Mtendaji wa mfumo wa E-Audit Next amesema mfumo huo umeanzishwa kwa lengo la kuwawezesha wakaguzi wa ndani wa hesabu kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia duniani, kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao pamoja na kupunguza gharama zinazotokana na shughuli za ukaguzi.
Amesema matumizi ya mfumo huo yanawawezesha wakaguzi kufanya baadhi ya majukumu yao kwa njia ya kidijitali, hatua inayosaidia kuongeza ufanisi, kuokoa muda na kuboresha namna taarifa za ukaguzi zinavyokusanywa, kuchambuliwa na kuhifadhiwa.
Amesema kampuni hiyo pia imekuwa ikitoa mafunzo bila malipo kwa wakaguzi wa ndani, kutokana na kubaini kuwa baadhi yao bado hawajaweza kutumia kikamilifu mifumo ya kidijitali katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kilatu ameongeza" kwa sasa mfumo wa E-Audit Next unahudumia kampuni za kibiashara, taasisi za kibenki pamoja na asasi za kiraia, huku akieleza kuwa lengo ni kuendelea kuwafikia wadau wengi zaidi wanaohitaji huduma za ukaguzi wa ndani unaotumia teknolojia"
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment