Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi amewataka wananchi kutokubali kutumiwa katika kuvuruga amani ya nchi, akiwaasa kuwa waangalifu na ajenda wanazoambiwa kuzibeba.
Kihongosi ametoa kauli hiyo , Jumamosi Septemba 19, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mbagala, Temeke jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema amani ni msingi wa shughuli zote za maendeleo na kwamba wananchi wanapaswa kuilinda kuanzia ngazi ya mtaa, wilaya, mkoa hadi Taifa.
“Tusije tukaruhusu hata kwa sekunde watu wakaichezea amani ya nchi yetu, tulinde amani kuanzia ngazi ya mtaa, Wilaya hadi Mkoa na Taifa,” amesema.
Amesema CCM imekuwa ikihimiza wananchi kulinda amani kwa kuwa bila amani shughuli za kijamii na kiuchumi haziwezi kuendelea kama kawaida.
Kihongosi amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa wanaowataka kuingia kwenye migogoro au vurugu si lazima wawe sehemu ya madhara yatakayojitokeza, akiwataka kutobeba ajenda wasizozielewa.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment