Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amezitaka taasisi za dini kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kutoa mafundisho yanayojenga jamii yenye ukarimu, upendo, utulivu, mshikamano na amani.
Dk Mwigulu alitoa kauli hiyo jana wakati wa ibada kuu ya kufunga Mkutano wa Makambi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa mikutano na makambi ya dini yana umuhimu mkubwa katika kuwakutanisha watu, kuwajengea uwezo, kubadilishana mawazo na kuwasaidia kuishi sambamba na mafundisho ya Mungu.
Alisisitiza kuwa taifa bora na la watu wema haliwezi kupatikana kama halitafanya mambo yanayofanywa na makambi hayo yanayowakutanisha watoto kutoka maeneo mbalimbali na kuwapatia malezi bora ya kujenga taifa lenye maadili na hofu ya Mungu.
Aliongeza kuwa mafanikio hayo hayaletwi na serikali pekee bali yanategemea jinsi jamii zinavyoandaliwa, akibainisha kuwa baadhi ya watu hudhani taifa bora hujengwa na serikali au nguvu za kijeshi wakati jamii yenye maadili ndiyo msingi muhimu wa taifa lenye heshima.
Katika kuimarisha ushirikiano huo, Dk Mwigulu alieleza kuwa serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa kila Mtanzania bila kujali dhehebu au taasisi ya dini, na itaendelea kushirikiana na makanisa pamoja na taasisi nyingine za dini ili kuhakikisha mshikamano unaimarishwa katika ujenzi na ustawi wa jamii.
Pia, alisisitiza umuhimu wa haki na uwajibikaji kwa kuwataka wananchi kila mmoja katika eneo lake kutimiza wajibu wa kusimamia haki za wengine, huku akiongeza kuwa Tanzania inajivunia uadilifu katika utumishi wa umma ambao kwa kiasi kikubwa unatokana na mafundisho bora ya kidini.
Aliwataka wazazi na walezi kuwa mstari wa mbele katika kutoa malezi bora kwa watoto, akisisitiza kuwa suala la malezi na maadili haliletwi na serikali pekee bali linahitaji jamii iliyotengenezwa kupitia taasisi za dini na viongozi wake, huku akiwakumbusha viongozi hao kuendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda na kudumisha amani ambayo ni kwa ajili ya Watanzania wote wakiwemo viongozi, serikali na jamii.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment