
Mufti Afafanua EDA ya Rais Samia Baada ya Kufiwa na Mumewe
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anaweza kuendelea kutekeleza majukumu muhimu ya Kitaifa licha ya kuwa katika kipindi cha eda baada ya kufiwa na Mumewe, Hafidh Ameir Hassan.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo Septemba 9, 2026 Jijini Dar es salaam, Mufti Zubeir amesema kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, Mwanamke aliyefiwa na Mume anatakiwa kukaa eda, hivyo sharti hilo linamhusu pia Rais Samia.
Mufti Zubeir amesema nafasi au wadhifa wa Mtu katika Jamii hauondoi masharti ya kidini yanayomhusu kama Muislamu, hivyo licha ya Rais Samia kuwa Mkuu wa Nchi mwenye majukumu ya Kitaifa, suala la eda linapaswa kuzingatiwa kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment