" Rais wa Marekani, Donald Trump Kutoa Milioni 13 Kwa Kila Raia wa Marekani

Rais wa Marekani, Donald Trump Kutoa Milioni 13 Kwa Kila Raia wa Marekani

 

Rais wa Marekani, Donald Trump Kutoa Milioni 13 Kwa Kila Raia wa Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump, ameahidi kutoa dola 5,000 (takribani TSh. Milioni 13.2) kwa kila raia mtu mzima wa Marekani iwapo Chama cha Republican kitafanikiwa kushinda na kudhibiti Baraza la Wawakilishi pamoja na Seneti katika uchaguzi wa katikati ya muhula utakaofanyika Novemba 2026.

Trump alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa Republican mjini Dallas, Texas, akisema malipo hayo yatakuwa kama “dividend” kwa wananchi kutokana na kile alichodai kuwa ni mafanikio makubwa ya kiuchumi ya Marekani.

Aidha, Trump amesema fedha hizo zitakuwa na sharti kwamba zitatakiwa kutumika ndani ya Marekani.

Hata hivyo, hakutoa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha fedha hizo au namna mpango huo utakavyotekelezwa. Vyombo vya habari vimeeleza kuwa mpango huo unaweza kugharimu zaidi ya dola trilioni moja, na hivyo kuibua maswali kuhusu uwezekano wake wa kutekelezwa.

 PROFESSOR MGOKO SERIES (EP 1)

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post