Na Woinde Shizza, ArushaKanisa la Ngurumo ya Upako lililopo Kisongo, jijini Arusha, linatarajia kumpokea Nabii Mkuu Prof. Geordavie Septemba 27, mwaka huu, katika ibada maalum itakayoambatana na uzinduzi wa kitabu chake kipya chenye maudhui kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.Tukio hilo linatarajiwa kukutanisha waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini Tanzania pamoja na wageni kutoka nje ya nchi, huku maandalizi yakiwa yameanza kukamilishwa kwa ajili ya ibada hiyo.Prof. Geordavie anatarajiwa kurejea Kisongo baada ya kuwa nje ya nchi akitekeleza majukumu ya huduma, huku kurejea kwake kukielezwa kuwa sehemu ya utaratibu wa kila mwezi wa kuhudhuria ibada katika kanisa hilo.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, msemaji wa Nabii Mkuu, Dr. Willy Ackyoo, alisema licha ya Prof. Geordavie kuwa na majukumu ya huduma katika maeneo mbalimbali duniani, ameweka utaratibu wa kurejea Kisongo kila mwezi kwa ajili ya ibada.“Prof. Geordavie ana huduma kubwa kimataifa, lakini ameweka utaratibu wa kuhudhuria ibada hapa Kisongo kila mwezi ,Septemba 27 ni moja ya ibada hizo muhimu,” alisema Dr. Ackyoo.Alisema maandalizi ya kumpokea Nabii huyo yamekamilika kwa kiasi kikubwa, huku waumini kutoka mikoa mbalimbali nchini wakitarajiwa kufika kushiriki ibada hiyo.Kwa mujibu wa Dr. Ackyoo, zaidi ya wageni 40 kutoka Ethiopia wanatarajiwa kuhudhuria, sambamba na wageni wengine kutoka nchi za Ulaya, Marekani na Australia.Mbali na ibada, uzinduzi wa kitabu kipya cha Prof. Geordavie ni miongoni mwa matukio yanayotarajiwa kuwa sehemu muhimu ya siku hiyo.Dr. Ackyoo alisema kitabu hicho kina maudhui kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza, hatua inayolenga kuwafikia wasomaji wanaotumia lugha hizo ndani na nje ya Tanzania.Alisema matumizi ya lugha hizo mbili yanaongeza wigo wa wasomaji na kuwezesha ujumbe uliomo kwenye kitabu kuwafikia watu wa makundi mbalimbali.“Kitabu hiki ni zawadi kwa Watanzania ,Ujumbe umeletwa kwa lugha ya Kiswahili ili kila mtu aweze kuuelewa,” alisema.Akizungumzia mwaliko kwa umma, Dr. Ackyoo alisema waumini na wageni kutoka maeneo mbalimbali wanakaribishwa kushiriki ibada hiyo, huku maandalizi ya chakula yakifanyika kwa ajili ya washiriki.Alisema tukio hilo linatarajiwa kuwa na ujumbe na matukio mbalimbali yatakayolenga kuwafikia washiriki kwa namna tofauti.“Mtu anayeingia kanisani hapa hawezi kutoka bure ,Mtu akikanyaga tu kanisani hapo hatatoka alivyo. Tunawasihi watu mbalimbali kuhudhuria,” alisema.Kauli hiyo imeambatana na kauli mbiu ya tukio hilo inayosema “Maneno Machache, Kazi Kubwa Zaidi.”Kwa mujibu wa waandaaji, ibada hiyo pamoja na uzinduzi wa kitabu vinatarajiwa kufanyika Septemba 27 katika Kanisa la Ngurumo ya Upako, Kisongo, jijini Arusha.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment