" NAIBU WAZIRI AVUTIWA NA USAJILI WANACHAMA KIDIGITALI, AITAKA NHIF KUONGEZA KASI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

NAIBU WAZIRI AVUTIWA NA USAJILI WANACHAMA KIDIGITALI, AITAKA NHIF KUONGEZA KASI YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

‎NAIBU Waziri wa Afya, Mhe Dkt. Florence George Samizi (Mb), amelipongeza Baraza la Wafanyakazi la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwa moja ya mabaraza bora nchini. Amelitaka baraza kuhakikisha ajenda ya Bima ya Afya kwa wote inawafikia wananchi wengi zaidi.

Nimefurahi kusikia kwamba katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/2026 Mfuko umeweza kufikia 10.7% ya Wananchi toka 8% ya wananchi iliyodumu kwa takriban miaka 10. Pamoja na pongezi hizo Mh. NAIBU WAZIRI ameutaka Mfuko kutumia TEHAMA na kusajili wanachama wengi zaidi ili kutimiza ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwafikishia wananchi wote huduma za bima ya afya. Hii itasaidia wananchi kuondokana na umaskini pale wanapopata maradhi. ‎Dkt. Samizi ametoa maelekezo Hayo wakati wa mkutano wa nne wa wa Baraza la 4 wafanyakazi NHIF, Jijini Arusha, na kusisistiza menejimenti ya wafanyakazi wa NHIF kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia uadilifu, weledi na uwajibikaji, huku wakisikiliza na kutatua kwa wakati kero za wananchi. ‎Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima ya afya. Kutoa huduma bora na kuwa na mfumo wa kupokea mrejesho toka kwa wananchi. ‎Katika kuelekea maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa NHIF, Dkt. Samizi amesema ni muhimu mfuko huo kuonesha mafanikio yaliyopatikana. Kuwepo kwa NHIF kumesaidia kuboresha huduma za Afya kwa kulipa madai na kutoa mikopo kwa vituo vya afya. Ni vema wanachi wakajulishwa hatua kubwa iliyofikiwa katika huduma za Afya na mchango wa NHIFkatika Sekta hii muhimu. Mlianza na vituo vichache sana mwaka 2001 hivi sasa yaani mwaka wa Fedha 2025/26 mmesajili zaidi ya vituo 10,600 nchi nzima. Ni vema kuonesha namna mlivyokabiliana na changamoto za wakati ule na namna zilivyowasaidia kuboresha Mfuko katika utoaji wa huduma. ‎Amesema mafanikio hayo yanadhihirishwa na kujituma, ushirikiano, umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa NHIF ili kufikia malengo ya mfuko kwa lengo la kutekeleza jitihada za Serikali za kuhakikisha wananchi wanapata bima ya Afya. ‎Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka, ameeleza mafanikio yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kilipa madai toka zaidi ya siku 90 hadi wastan wa siku 50 kwa mwaka wa Fedha 2025/2026. Vile vile alieleza kwamba Mfuko umeendelea kuimarika ambapo ziada imeongezeka kwa 57% Mfuko umepunguza matumizi kwa asilimia13% na uwekezaji umeongezeka kwa 106%.

Hii imewezesha Mfuko kuendeleza kifurushi cha wanafunzi, Toto Afya. Mfuko kusajili kifurushi cha tarangire, Mikumi, Ngorongoro, Serengeti Tanzanite na kifurushi cha vikundi yaani Umoja Afya ambacho ni sh. 60, 000 kwa matibabu ya mwaka mzima.

Vile vile alielezea mikakati inayotekelezwa na mfuko huo katika kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na matumizi ya TEHAMA kwenye usajili, uchakataji madai na kupambana na udanganyifu. Mfuko pia unashirikisha Sekta Binafsi katika usajili wa wanachama na katika huduma za matibabu. ‎Mwakilishi wa chama Cha wafanyakazi TUGHE, Bw.Paul wamepongeza baraza Hilo kuzingati misingi ya Kazi stahiki za wafanyakazi kwenye taasisi hiyo. ‎Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki semina elekezi ya siku mbili wamesema wamepata maarifa na mwelekeo mpya ambao utawasaidia kuboresha utendaji wao wa kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.

Bima ya Afya kwa wote! Jiunge sasa!

Post a Comment

Previous Post Next Post