
Wakati Tanzania ikiendelea kukumbuka kipindi kigumu cha kihistoria kilichofuata kifo cha ghafla cha Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli, mnamo Machi 19, 2021, uongozi wa nchi umeendelea kuimarika chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia misingi ya amani, uwezeshaji wa kidiplomasia, na mageuzi makubwa ya kiuchumi.
Kupitia mwongozo wa wazi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Dkt. Samia aliapishwa kuwa Rais mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi, akichukua kijiti katika mazingira ya kipekee na kugeuza sintofahamu ya awali kuwa matumaini mapya kwa wananchi.
Kabla ya kushika wadhifa huo wa juu, Dkt. Samia alijijengea uzoefu mpana wa kisiasa na kiutawala tangu kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1987, uzoefu uliomwezesha kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya serikali na chama, pamoja na kuwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini katika jopo la Umoja wa Mataifa lililohusika na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.
Uzoefu huo uliweka msingi thabiti wa mtazamo wake wa uongozi unaozingatia ushirikishwaji na ujasiri katika kusimamia uwajibikaji wa umma, mapambano dhidi ya rushwa, na utoaji wa haki bila kuvumilia uzembe.
Uwezo wake wa kiuongozi ulidhihirishwa tena alipochaguliwa rasmi na wananchi kushika usukani wa nchi katika uchaguzi mkuu kupitia tiketi ya CCM, ambapo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilimtangaza mshindi kwa kura nyingi zilizompa mamlaka ya kuiongoza awamu ya sita.
Chini ya uongozi wake, Tanzania imeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta za kipaumbele zikiwemo elimu, afya, miundombinu, na huduma za jamii, sambamba na usimamizi madhubuti wa uteuzi wa viongozi wa kitaifa uliofanyika kwa utulivu na bila misukosuko ya kisiasa.
Katika kujenga mshikamano wa kitaifa, Rais Samia anatumia falsafa yake ya 4R inayojumuisha Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi, na Ujenzi mpya wa taifa.
Hivi karibuni, Julai 30, 2026, alifanya mazungumzo rasmi na viongozi wa vyama vya siasa katika Ikulu ya Dar es Salaam ili kuimarisha amani na mshikamano. Juhudi hizo za siasa za kistarabu zimekwenda sambamba na uundaji wa Tume ya Haki Jinai ili kuboresha mifumo ya kisheria nchini.
Katika nyanja ya kimataifa, serikali imeweka msisitizo mkubwa kwenye diplomasia ya uchumi, hatua iliyofungua milango ya ushirikiano na taasisi za kifedha, nchi mbalimbali, na mashirika ya kimataifa, huku Tanzania ikiendelea kuwa mwenyeji wa mikutano mikubwa ya kimataifa na kuimarisha nafasi yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na eneo huru la biashara barani Afrika.
Kupitia ushiriki wake katika filamu ya The Royal Tour, utalii wa Tanzania umezidi kutangazwa duniani kote.
Sambamba na hayo, utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati umeendelea kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi, ikiwemo Mradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), na Daraja la Kigongo-Busisi, miradi ambayo imethibitisha utashi imara wa kisiasa katika kuleta maendeleo ya kudumu.
Ni dhahiri kwa siaza zake za kistaarabu,uongozi wake umeendelea kuwa chachu ya usawa wa kijinsia, ukiwahamasisha wanawake kushika nafasi za juu za maamuzi na kuhakikisha ushiriki wao unachangia kikamilifu katika ustawi wa taifa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment