Na, Egidia Vedasto,
Misalaba Media, Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kutekeleza malengo yake ya kuimarisha sekta ya afya kwa kuongeza uwekezaji katika huduma za afya ya msingi.
Akifungua Mkutano wa II wa Kimataifa wa Afya ya Msingi unaofanyika jijini Arusha kwa siku 3, unaowashirikisha washirika zaidi ya elfu tatu kutoka ndani na nje ya nchi akimuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na zinazopatikana kwa urahisi bila kujali hali zao za kiuchumi.
Aidha Dkt. Nchemba amesema Serikali imeweka mkazo pia katika kuimarisha uzalishaji wa dawa nchini. Amesema ujenzi wa viwanda vya dawa utawezesha kupunguza utegemezi wa dawa kutoka mataifa ya nje na kuongeza uwezo wa nchi kujitegemea katika sekta ya afya.
Vile vile amesema Tanzania inaendelea kuweka mbele malengo yake ya ndani ya maendeleo ambayo yanaendana na malengo ya kimataifa ya kuboresha afya ya wananchi.
"Matumizi a nafasi hii kuwaomba washirika wa maendeleo kuunga mkono mipango hiyo kwa kushirikiana na Serikali katika kuondoa vikwazo vinavyoweza kumzuia mtu anayehitaji huduma za afya kuzipata kwa wakati na kwa ubora unaostahili"
Hata hivyo Dkt. Mwigulu amesema Serikali imeanza kutekeleza mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, hatua inayolenga kupanua wigo wa wananchi wanaoweza kupata huduma za afya bila kukabiliwa na changamoto kubwa za gharama. Ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetoa ajira kwa watumishi wa afya 16,000, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza nguvu kazi katika vituo vya afya nchini.
Licha ya hayo ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya afya katika maeneo mbalimbali nchini, ikiwemo ujenzi wa nyumba zaidi ya 430 za watumishi wa afya ndani ya miaka minne.
Katika namna hiyohiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Prof. Riziki Shemdoe, amesema Tanzania inalenga kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kwa kuzingatia azma ya dunia ya kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afya ya msingi.
Prof. Shemdoe amesema mkutano huo unalenga kutathmini maendeleo yaliyofikiwa katika utoaji wa huduma za afya ya msingi, hususan katika mazingira yenye changamoto za upatikanaji wa rasilimali za kutosha.
Ameongeza kuwa, mkutano huo pia ni fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu, kujadili fursa na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto zinazokabili sekta hiyo.Amesema Tanzania imeendelea kuongeza juhudi na uwekezaji katika huduma za afya ya msingi, jambo linaloonekana kupitia idadi kubwa ya wananchi wanaotumia vituo vya afya vilivyo karibu na makazi yao.
Kwa mujibu wa takwimu alizozitoa, kati ya wanawake wajawazito milioni 2.09 waliojifungua, asilimia 95.9 walitumia vituo vya afya ya msingi.
Aidha, Prof. Shemdoe amesema kati ya mahudhurio milioni 32.5 ya wagonjwa wa nje nchini, asilimia 86 walipata huduma katika vituo vya afya ya msingi. Takwimu hizo, amesema, zinaonesha umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha vituo vya afya ya msingi ili viweze kutoa huduma bora, salama na zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
Vilevile amesema kuwa kati ya vituo 8,288 vya afya vinavyomilikiwa na Serikali nchini, vituo 7,946 sawa na asilimia 95.8 vinamilikiwa na Halmashauri. Kwa msingi huo, amesema Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano, uwekezaji na mikakati ya kuboresha afya ya msingi, sambamba na kuimarisha usalama wa afya na diplomasia ya afya ndani ya Afrika na duniani kwa
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment