Wafanyabiashara wanaotumia mitandao ya kijamii kujitangaza wametakiwa kuwekeza katika utengenezaji wa maudhui yenye ubora na mvuto ili kuongeza ushawishi kwa wanunuzi, badala ya kutegemea idadi kubwa ya wafuasi pekee.
Rai hiyo imetolewa na mtaalamu wa maudhui ya mitandao ya kijamii kutoka Kampuni ya Distinctsocials ya Sinza Kijiweni, Dar es Salaam, Basili Pasience, alipozungumza na moja ya magazeti makubwa nchini hivi karibuni.
Alibainisha kuwa siri kuu ya kuvuta wateja na kufanya biashara kubwa mtandaoni iko kwenye jinsi bidhaa inavyowasilishwa na kusisimua hadhira.
Pasience alieleza kuwa kuwa na idadi kubwa ya wafuasi hakuhakikishii mauzo ya juu, kwani wateja hufanya maamuzi ya kununua au kuagiza bidhaa wakitokea kuvutiwa na ubora wa maudhui yaliyowasilishwa.
Alishauri wafanyabiashara kutumia vizuri mifumo kama vile Instagram na Facebook kwa kutumia mikakati madhubuti, ikiwemo kuwa hai katika kujibu maswali na maoni ya wateja, sambamba na kutumia matangazo ya kulipia ili kufikia wigo mpana zaidi wa wanunuzi.
Aidha, mtaalamu huyo alikemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kupakia bidhaa nyingi kwa pamoja kwenye mfumo wa WhatsApp Status, akieleza kuwa mtindo huo huwachosha wateja na kuondoa hamu ya kutazama.
Alisisitiza badala yake kuandaa ujumbe au picha moja yenye mvuto na ushawishi mkubwa kwa mnunuzi, badala ya kujaza kurasa kwa wakati mmoja
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment