" TUICO Yaonya teknolojia bila maarifa na uzalendo

TUICO Yaonya teknolojia bila maarifa na uzalendo




CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) kimeipongeza serikali na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kukamilisha mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) lenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115.

Pongezi hizo zilitolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Sylvester Mrope mjini Morogoro kwenye mkutano wa Jukwaa la 17 la viongozi wa Tuico na Tanesco, ambapo alisisitiza kuwa teknolojia pekee haitoshi bila wafanyakazi wenye maarifa, nidhamu na uzalendo, huku akishauri shirika hilo kuendelea kuwaongezea ujuzi wafanyakazi kupitia mifumo ya kielektroniki na kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kupikia.

Katika mkutano huo uliowashirikisha viongozi mbalimbali, Kaimu Mkuu wa Sekta ya Biashara wa TUICO Taifa, Prosper Mrema alieleza kuwa jukwaa hilo lilitumika kutoa mafunzo ya maadili ya utumishi wa umma na majukumu ya viongozi wa matawi, wakati Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Tuico na Tanesco, Janet Vesso alibainisha kuwa majadiliano na mwajiri yamewezesha wafanyakazi wengi kupandishwa madaraja, kuboreshewa maslahi na kupatiwa vitendea kazi vikiwemo magari.

Post a Comment

Previous Post Next Post