Shule ya Green View ya Jijini Mwanza lmeendelea kuonesha ubora wake kwa kuhimiza wanafunzi wake kuweka jitihada katika masomo ya amali ili waweze kuwa uwezo wa kufanya shughuli za uzalishaji mali.
Hayo yamebainishwa leo jijini Mwanza katika mahafali ya wanafunzi wake waliohitimu darasa la saba mwaka huu.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Kasanzu Masunga alisema wanajitahidi wanafunzi kuwawezesha kufahamu vizuri masomo yanayowawezesha kujitegemea mara wamalizapo shule ya msingi.
Alisema wanafunzi 48 wamehitimu darasa la saba ambapo 26 ni wa kike wakati 22 wakiwa ni wavulana ambawo wameandaliwa vizuri kuweza kujiunga na masomo ya sekondari.
Diwani wa Kata ya Isamilo Jijini Mwanza Charles Nyamasiriri alihimiza wazazi kuweka jitihada katika kuwezesha watoto wao wasome kwani urithi kwa sasa ni wa elimu.
Alishukuru kuwepo kwa masomo yanayowajengea wanafunzi maarifa ya kuwa wabunifu kwani hatua hiyo ni mhimu kuweza kuwa na watanzania wenye umri mdogo wanaoweza kujitegemea.
Mama Pendo Hemela ambaye mtoto wake Glory Geofrey amehitimu alishukuru mwanaye kuhitimu na hivyo kutoa wito kwa wanafunzi kuendeleza yale mema waliyojifunza shuleni hapo.
Alisema kuwepo kwa masomo yanayowaandaa watoto kuendana na majitaji ya sasa duniani ni hatua nzuri ya kujenga kizazi bora cha watu wakaojiajiri wenyewe.
Post a Comment