Watendaji wa Halmashauri ya Mji Kasulu wameungana kuukaribisha Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili Halmashauri ya Mji Kasulu tarehe 10 Septemba 2026, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa mbio za Mwenge wa Uhuru nchini.Katika maandalizi hayo , watendaji hao wamebeba mabango yenye ujumbe unaoainisha baadhi ya Miradi itakayotembelewa na Mwenge ikiwemo Ofisi ya Mtendaji wa Mtaa wa Mugandazi, Mradi wa Maji Miji 28, Mabwawa ya Samaki Musambara, Wodi ya Wazazi na Chumba cha Upasuaji Mwami Ntale, taa za barabarani, vyumba viwili vya madarasa Shule ya Sekondari Mwilamvya Mpya pamoja na jengo la ghorofa la Kituo cha Afya Victorian (Kwa Kabadi).Halmashauri ya Mji Kasulu inaendelea kujiandaa kwa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kwa kuhakikisha watumishi na wananchi wanashiriki kikamilifu katika mapokezi ya Mwenge ili kupata fursa ya kufahamu na kushuhudia utekelezaji wa miradi ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254










Post a Comment