Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha Halmashauri ya Mji Kasulu kimefanya kikao cha kujadili na kuweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wa shughuli za kilimo, mifugo na uvuvi, pamoja na kukabiliana na changamoto zinazoweza kuathiri uzalishaji kuelekea kipindi cha masika.Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Sabinus L. Chaula, ambapo wataalamu wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Nino, fursa za mikopo kwa vijana, chanjo za mifugo pamoja na ukaguzi wa nyama.Aidha, wataalamu hao wamejadili kwa kina upatikanaji wa pembejeo za kilimo ili kurahisisha upatikanaji wa mbolea za ruzuku na mbegu bora za mahindi kwa lengo la kuongeza uzalishaji na tija katika sekta ya kilimo.Kikao hicho pia kimejadili umuhimu wa kubaini maeneo yaliyopo na kutafuta maeneo mapya kwa ajili ya ukusanyaji wa mazao, kutoa elimu kwa jamii kuhusu uzalishaji wa mazao ya chakula, mbogamboga, matunda na kutambua maeneo yanayofaa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.Katika hatua nyingine, Chaula amewasisitiza Maafisa kilimo, mifugo na uvuvi kufanya kazi kwa bidii, kusimamia ipasavyo maeneo yao ya kazi na kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili kuimarisha uzalishaji katika sekta hizo.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment