kampuni ya Huduma za Simu ya mikononi Yas imewajengea uwezo mawakala wake toka wilaya ya Ilemela na Nyamagana Jijini Mwanza juu utoaji huduma zao kwa Mixx by yas ili waweze kupata manufaa zaidi.
Tukio hilo lilienda sambamba na utoaji wa zawadi kwa mawakala waliofanya vizuri kazi zao katika maeneo tofauti Jijini hapa.
Akizungumza leo na mawakala 448 jijini Mwanza, Aisha Kisai Wakala Specialist alisema zipo kamisheni 13 hivyo ni jukumu la mawakala kujituma zaidi kuweza kuongeza kipato chao.
Aliwataka vilevile mawakala kujihadhari na tishio la wizi kupitia njia ya utakatishaji fedha unaofanywa kupitia huduma zinazofanywa kwa mawakala katika maeneo yao.
Meneja wa Yas Mkoani Mwanza Abdillahi Luhorela alisema katika kongamano hilo wamewafundisha mawakala wa fedha namna ya kukuza mitaji yao kwa njia uwekaji wa akiba.
Alisema watakuwa wakitoa motisha kwa mawakala wanaofanya vizuri ili kuwajengea motisha ya ufanyaji kazi zao kwa juhudi na maarifa.
Naye Nelson Jackson wa Mtaa wa Uhuru alisema huduma ya fedha ya Mix by yas huwawezesha kupata motisha ya bonasi kw kushawishi uwekaji wa akiba za fedha kwenye akaunti. "Najivuna kupata mara kwa mara motisha ya namna hiyo".
Wakala wa Mixx by Yas toka Nyambiti wilayani Ilemela Edwin Chrispo alisema anapata faida kwa kuuza kuuza vifurushi mbalimbali vinavyotolewa kupitia kwenye mtandao huo akitaja luku, ada za shule na kukata tiketi kwa njia ya basi.
Aidha Mariam Isaack toka Sinai Maduka Tisa alishukuru kuwepo kwa tukio hilo la kongamano kwani limewawezesha kupata maarifa na ufumbuzi kwa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawasibu.
Alisema mbinu za kujihadhari na matukio machafu ya utakatishaji wa fedha na namna ya kujihadhari ni mojawapo ya mbinu walivyoelezwa namna kukabiliana nayo ili waweze kutoa huduma zao vizuri kwenye jamii.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 2
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652
Post a Comment