Na Lydia Lugakila Misalaba media,
Mbeya
Shule ya Sekondari Airport iliyopo Mkoani Mbeya imefanya Mahafali ya 18 ya Kidato cha nne huku ikiweka mikakati kabambe ya kuboresha taaluma, ikiwemo kukamilisha mada kwa wakati na kudhibiti utoro darasani kwa asilimia 100.
Akizungumza katika mahafali hayo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Airport, Ayubu Malambugi, alisema kuwa shule imejiwekea mikakati ya kufuata mtaala wa kukuza ujuzi na umahiri, kufanya mitihani ya kujipima na shule jirani, kutoa motisha kwa wanafunzi wanaofanya vizuri, na kusimamia vipindi vya dini ili kujenga nidhamu na maadili.
Ayubu alibainisha kuwa shule pia imeweka utaratibu wa kusaidia kutatua changamoto za wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu ili kuzuia kushuka kwa taaluma yao.
Aidha akisoma risala ya shule, Mkuu huyo wa shule alitaja changamoto kubwa inayowakabili kuwa ni baadhi ya wazazi na walezi kutolipa ada kwa wakati, hali inayokwamisha uendeshaji wa shule na kusababisha wanafunzi kupoteza vipindi vya masomo pindi wanapofuatiliwa ada.
"Tunawasihi wazazi na walezi kulipa ada kwa wakati ili kuondoa usumbufu" alisema mkuu wa shule ya Airport.
Pia katika changamoto nyingine aliongeza kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa hawatoi ushirikiano wa kutosha katika kufuatilia maendeleo ya taaluma na nidhamu ya watoto wao," alisema Ayubu, huku akiwashukuru wazazi wanaotimiza wajibu huo bila usumbufu.
Mkuu wa shule hiyo aliwataka wazazi kuendelea kuwatia moyo na kuwaombea wanafunzi wanaotarajia kuanza mitihani yao ya kitaifa Oktoba 19, 2026, pamoja na kuwa mabalozi wema wa kuisemea vizuri shule hiyo.
Naye Mgeni Rasmi katika mahafali hayo, Afisa Kata ya Iyela, Nsajigwa Mwakapala, alimshukuru Mkurugenzi wa shule hiyo, Nikuswiga Malambugi, kwa maono yake ya kuanzisha taasisi hiyo iliyoongeza thamani katika Kata ya Iyela na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutengeneza ajira.
Mwakapala aliutaka uongozi na walimu kusimamia kikamilifu mikakati waliyojiwekea, ikiwemo uthibiti wa utoro na usahihishaji wa mitihani kwa wakati ambapo pia, aliwaasa wazazi kuwarithisha watoto wao elimu na maadili mema, akionya kuwa nidhamu ya watoto wa kiume imeporomoka kwa kiasi kikubwa hivi karibuni.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Shule hiyo, Nikuswiga Malambugi, aliwashukuru wazazi wote wanaolipa ada kwa wakati na kuahidi kuendelea kuwekeza ili kuifanya shule hiyo kuwa kituo cha mfano cha elimu bora.
Shule ya Sekondari Airport inamilikiwa na shirika binafsi la ISRANI chini ya Mkurugenzi Nikuswiga Malambugi ambapi shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2006 na inasomesha wanafunzi wa kutwa na bweni kwa wavulana na wasichana.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment