Na Lydia Lugakila Misalaba media,MbeyaSerikali mkoani Mbeya imeeleza kuvutiwa na mwekezaji kutoka nchini China aliyewekeza katika sekta ya biashara na huduma kupitia Hometan Supermarket, baada ya kuonyesha uaminifu wa kulipa kodi bila usumbufu pamoja na kuendelea kutoa huduma na bidhaa zenye ubora.Kauli hiyo ya Serikali imekuja kufuatia maadhimisho ya mwaka mmoja wa utoaji wa huduma kwa wananchi na wateja wa mkoa huo na mikoa ya jirani, hafla iliyofanyika Oktoba mwaka huu katika eneo la Kabwe, mkoani Mbeya.Akisoma risala katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo kutoka nchini China, Kingsley Who, alielezea safari ya mwaka mmoja na mafanikio waliyoyapata, huku akisema kuwa wamepata ushirikiano mkubwa kutoka Serikali ya Mkoa na Wananchi, jambo lililowapa moyo wa kuendelea kuwekeza zaidi. Who ameahidi kuendelea kuboresha huduma na kuongeza bidhaa ili kila mteja anayehudumiwa apate huduma bora, huku akibainisha kuwa mwaka 2027 utakuwa wa mafanikio makubwa zaidi kuliko mwaka 2026 katika huduma."Asante sana wateja wetu kwa upendo mliouonyesha kwa kutuamini na kutumia bidhaa zetu mmetukubali sana," alisema Who.Akizungumza katika hafla hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya, Bi. Devotha Chacha—aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Solomon Itunda alipongeza huduma zinazotolewa na duka hilo. Alieleza kuwa supermarket nyingi zilizoanzishwa hapo awali zilifungwa kutokana na kukosa sifa, bidhaa duni, na uendeshaji usioridhisha, lakini Hometan Supermarket imekuwa mfano wa kuigwa mkoani humo na imeleta mapinduzi makubwa.Bi. Devotha aliongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameweka mazingira mazuri na milango wazi kwa wawekezaji hivyo, aliwaomba Wananchi wenye maeneo ya uwekezaji ambayo hayajatumika wayatoe ili kuwaruhusa wawekezaji. Pia, alimhimiza mwekezaji huyo kuangalia uwezekano wa kufungua kiwanda cha maji, kwani uhitaji wa maji bado ni mkubwa mkoani Mbeya.Alisitiza kuwa Serikali ya Mkoa wa Mbeya itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha, kwani Tanzania na China ni nchi zenye ushirikiano mzuri.Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga aliwapongeza wawekezaji hao kwa kutoa huduma bora na nafuu kwa Wananchi katika mazingira ya utulivu.Kamanda Kuzaga amewaomba wawekezaji hao kuboresha mfumo wa usambazaji wa bidhaa ili kuwarahisishia huduma wateja walioko mbali, huku akiahidi kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kudumisha ulinzi na usalama katika eneo hilo na mkoa mzima.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254






Post a Comment