Maafisa usafirishaji katika Kijiji Cha Seseko kilichopo Kata ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kujiepusha na ajali za barabarani zinazoweza kuepukikaElimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Wilaya ya Shinyanga Koplo Elipendo Nadula ambapo amewaeleza kuwa kila afisa usafirishaji anatakiwa kufuata Sheria za usalama barabarani pasipo shuruti Kwa ni Kwa faida yake yeye na watumiaji wengine wa barabara Koplo Elipendo amewasisitiza kujisimamia wenyewe pamoja na kwamba wapo vijijini na sio kutekeleza Sheria mpaka pale watakapowaona Askari katika maeneo yao.Elimu hiyo ya usalama barabarani Kwa Maafisa usafirishaji vijijini inalenga kutokomeza ajali za barabarani katika maeneo yote na sio mijini tu.Kwa upande wao Maafisa usafirishaji hao wamelipongeza Jeshi la Polisi Kwa hatua hiyo ya kuwafikia madereva wa pikipiki waliopo vijijini kwani itasaidia kutokomeza ajali za barabarani vijijini kutokana na kuongezeka Kwa uelewa Kwa madereva hao.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 05
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment