Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga, SACP Janeth Magomi, amekutana na maafisa wa
usafirishaji wa bodaboda Kanda ya Maganzo, Wilaya ya Kishapu, na kuwataka
kuzingatia usalama, kutii sheria bila shuruti na kuepuka kujichukulia sheria
mkononi.
Kamanda
Magomi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 7, 2026, katika Uwanja wa Sabasaba, Kijiji
na Kata ya Maganzo, wakati akitekeleza programu ya “Ongea na Kamanda”, ambapo
akiwa ameambatana na maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali, alitoa
elimu kwa waendesha bodaboda kuhusu masuala mbalimbali ya usalama.
Katika
mkutano huo, Kamanda Magomi amewataka waendesha bodaboda kuweka usalama wao
mbele wakati wote, kutii sheria za nchi kwa hiari, pamoja na kudumisha amani na
utulivu, akisisitiza kuwa bila amani hakuna shughuli za uzalishaji mali na
maendeleo, ikiwemo shughuli za usafirishaji wa bodaboda.
Aidha,
amewataka kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha
msimu huu kwa kushiriki katika usafi wa mazingira, ikiwemo kusafisha mitaro ili
kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
Kamanda
Magomi pia amewakumbusha waendesha bodaboda kuhusu Kampeni ya Usalimishaji wa
Hiari wa Silaha Haramu, ambayo inatarajiwa kukamilika Oktoba 31, 2026, huku
akiwataka wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa
taarifa kwa vyombo vya dola pale wanapokutana na changamoto za kiusalama.
Katika hatua
nyingine, Kamanda Magomi amechangia Shilingi 100,000 kwenye mfuko wa wanachama
wa maafisa wa usafirishaji Kanda ya Maganzo, akihamasisha wanakikundi hicho
kuwa na chama kwa ajili ya kusaidiana katika shughuli mbalimbali za kijamii
zinazojitokeza miongoni mwao.
Kwa upande
wao, maafisa wa usafirishaji wamempongeza Kamanda Magomi kwa kufika katika eneo
hilo na kutoa elimu ya usalama, huku wakiahidi kutekeleza maelekezo aliyoyatoa.
Pia wameipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kushirikiana nao katika masuala
mbalimbali.
Hata hivyo,
wameiwasilisha changamoto ya kutopata leseni za kuendeshea vyombo vya moto,
wakieleza kuwa licha ya baadhi yao kusoma mafunzo na kupata vyeti, vyuo
walivyosoma havionekani au havijasajiliwa katika mfumo unaotumika.
Kufuatia
changamoto hiyo, Kamanda Magomi ameahidi kuwaunganisha na wakufunzi kutoka vyuo
vilivyosajiliwa ili wapate mafunzo kwa gharama nafuu, waweze kupata vyeti
vinavyotambulika na hatimaye kukamilisha taratibu za kukata leseni za
kuendeshea vyombo vya moto.


PROFESSOR MGOKO EPISODE 04
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment