Katika tukio la kihistoria na la furaha kubwa lililofanyika Jumamosi, tarehe 22 Novemba 2026, umati wa watu ulishuhudia Harusi iliyotikisa Kanda ya Ziwa, ambapo ilikabidhiwa zawadi ya Tsh 1,300,000,000/-. Hii Harusi ndiyo imefunga mwaka.
Zawadi hiyo ilitolewa kama Zawadi ya Kamati kwa Kishepo Peter Kishepo, ikiwa ni ishara ya upendo, mshikamano na kutambua mchango wake katika jamii.
Akizungumza wakati wa kutoa zawadi hiyo, MC wa Mchongo kutoka Kanda ya Ziwa, akitoa sifa za Katibu, amesema:
"Baada ya matumizi yote, baki ni kiasi cha Sh. Bilioni 1,300,000,000/=. Hii ndiyo chanji."
Katibu huyu anayesifiwa ni Peter Ndimila, ndiye amekuwa Katibu ambaye amekuwa akisimamia shughuli zote zinazotikisa Kanda ya Ziwa, shughuli zote zinazofanya vizuri na kukusanya michango kwa uaminifu mkubwa. Na amekuwa akijitolea bure.
Peter Ndimila ni mtu wa kuigwa. Ni kiongozi mwenye hekima, mchapakazi, mnyenyekevu, mkweli na mwenye upendo wa kweli kwa watu wake. Ni mtu anayesimama imara kwenye ukweli, anayeheshimu kila mtu, anayejitoa bila kuchoka na anayebeba dhamana ya watu kwa moyo wake wote. Kwa uaminifu wake, busara zake na utendaji wake mzuri, amekuwa nguzo imara ya umoja na mafanikio ya Kanda ya Ziwa.
Kauli hiyo ilitolewa na MC wa Mchongo kutoka Kanda ya Ziwa, na kuwafanya wote waliokuwepo kushangilia na kumshukuru Mungu kwa mafanikio hayo, huku wakimpongeza mpokeaji wa zawadi hiyo.
Lakini pia Kanda ya Ziwa imekuwa na Umoja ambao umekuwa mfano katika Nchi yetu ya Tanzania. Umoja huo umekuwa mfano na umekuwa ukiwakutanisha Wachimbaji wa Madini, Wafanya Biashara, Wakulima na Wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa. Hakika Umoja huu ni mfano wa kuigwa.
Tukio hilo linaendelea kuvuta hisia za Watanzania na kila mmoja kutamani kuja kuishi Kanda ya Ziwa.
Tukio hilo lilipambwa vizuri na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wengi.
Hongera sana Kishepo Peter Kishepo!
Mungu akubariki na akuzidishie.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 08
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment