" JIMOTOLI MADUKA ACHANGIA TSH. 100,000 KUKAMILISHA UPIMAJI WA SHULE YA SEKONDARI MILALA

JIMOTOLI MADUKA ACHANGIA TSH. 100,000 KUKAMILISHA UPIMAJI WA SHULE YA SEKONDARI MILALA

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, tarehe 21 Novemba 2026 amechangia kiasi cha Shilingi 100,000 kwa ajili ya kusaidia mchakato wa ukamilishaji wa upimaji wa Shule ya Sekondari Milala.

Mchango huo umetolewa kwa lengo la kusaidia kufanikisha mchakato huo, ambao ni sehemu ya hatua zinazohitajika katika maendeleo ya shule hiyo.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, amesema mchango wake wa Shilingi 100,000 ni kwa ajili ya kusaidia gharama za zoezi la ukamilishaji wa upimaji wa eneo la Shule ya Sekondari Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.


Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, akiwa ofisini kwake akitafakari kuhusu mustakabali wa Shule ya Sekondari Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, ambayo kwa mujibu wa maelezo yake haijaanza kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano. Ameeleza umuhimu wa wadau na jamii kuungana kuipambania shule hiyo kwa kutoa michango ya hali na mali pamoja na ushauri, ili kukamilisha upimaji wa eneo lake na hatimaye kupatikana kwa hati miliki ya eneo la shule. Karibuni tushirikiane kuunga mkono juhudi hizi kwa maendeleo ya elimu.

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Frank William Mgata, tarehe 21 Novemba 2026 akishiriki katika kikao cha kupokea mchango wa Shilingi 100,000 kutoka kwa Katibu wa Jumuiya hiyo, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, kwa ajili ya kusaidia gharama za ukamilishaji wa upimaji wa eneo la Shule ya Sekondari Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda. Ndg. Mgata amempongeza Katibu huyo kwa kuonesha uwajibikaji na kujitolea katika kuunga mkono mchakato huo wa maendeleo ya shule.

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, wakiwa katika utekelezaji wa majukumu yao wakati wa kupokea mchango wa Shilingi 100,000 uliotolewa na Katibu wa Jumuiya hiyo, Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, kwa ajili ya kusaidia gharama za ukamilishaji wa upimaji wa eneo la Shule ya Sekondari Milala, iliyopo Kijiji cha Milala, Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, Ndg. Pius M. Buzumalle, akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Frank William Mgata, wakati wa shughuli za jumuiya hiyo tarehe 21 Novemba 2026.

PROFESSOR MGOKO EPISODE 08

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post