
NA DENIS MLOWE, IRINGA
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini kimetangaza kifo cha Katibu wa Siasa na Uenezi wa wilaya hiyo, Ndugu Edo Bashir, aliyefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Ikonda, mkoani Njombe, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa iliyotolewa na CCM Wilaya ya Iringa Mjini, chini ya Mwenyekiti wa chama hicho, Said Rubbeya, imesema chama hicho kimepokea taarifa za kifo cha kiongozi huyo kwa masikitiko makubwa.
Edo Bashir alikuwa akihudumu katika nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini, nafasi yenye jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli za kisiasa na mawasiliano ya chama katika wilaya hiyo.
CCM Wilaya ya Iringa Mjini imesema taarifa zaidi kuhusu ratiba ya mazishi na mipango mingine ya kuaga mwili wa marehemu zitatolewa baadaye.
Kifo hicho ni pigo kwa chama hicho wilayani Iringa Mjini, huku wanachama na viongozi wakitarajiwa kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu.
Eddo Bashiri ambaye alikuwa mtangazaji maarufu wa Radio ebony fm na balozi wa makampuni mbalimbali ikiwemo mtandao wa simu wa Yas hadi anafariki ameacha watoto wawli mapacha.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 08
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment