" MBUNGE PATALI AUNGANA NA TARURA KUDHIBITI ATHARI ZA MVUA ZA EL NINO

MBUNGE PATALI AUNGANA NA TARURA KUDHIBITI ATHARI ZA MVUA ZA EL NINO

Na mwandishi wetu Misalaba media ,Mbeya

Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini, Patali Shida Patali, kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Mbeya, imefanya ziara ya kukagua maeneo korofi yanayoweza kuathiriwa na mvua kubwa za El Nino, kwa lengo la kubaini changamoto na kuweka mikakati ya mapema ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.

Akizungumzia lengo la ziara hiyo, Katibu wa Mbunge wa jimbo hilo, Emmanuel Mkoma, amesema hatua hiyo inalenga kufuatilia na kubaini maeneo yenye changamoto mbalimbali ambayo ofisi ya mbunge imekuwa ikipokea taarifa zake kutoka kwa wananchi, ili hatua stahiki zichukuliwe kabla ya mvua hizo kunyesha.

Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Mbeya, Mhandisi William Lameck, amesema maeneo yote yaliyobainishwa yanafanyiwa kazi kwa haraka, huku mkandarasi akipewa maelekezo ya kuyashughulikia ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.


Aidha, amewataka Wananchi kushiriki kikamilifu katika kudhibiti athari za mvua kwa kusafisha mitaro ya kupitisha maji na kuepuka kutupa taka ovyo, akieleza kuwa tabia hiyo husababisha kuziba kwa mitaro na hivyo kuzuia maji kupita kwa urahisi.

Nao baadhi ya wananchi wa maeneo yaliyotembelewa wameishukuru Ofisi ya Mbunge pamoja na wataalamu wa TARURA kwa kufika katika maeneo yao na kusikiliza changamoto zinazowakabili, wakieleza kuwa ziara hiyo imewapa fursa ya kuwasilisha kero ambazo kwa muda mrefu zimekuwa zikisababisha usumbufu katika maeneo yao.



PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment

Previous Post Next Post