" MCHUNGAJI KIPESHA AELEZA MAMBO YANAYOWEZA KUMZUIA MUUMINI KUINGIA KATIKA UWEPO WA MUNGU

MCHUNGAJI KIPESHA AELEZA MAMBO YANAYOWEZA KUMZUIA MUUMINI KUINGIA KATIKA UWEPO WA MUNGU



Na Lydia Lugakila Misalaba media ,Mbeya

Mchungaji wa Kanisa la Pentecostal Holiness Mission (PHM), lililopo Kata ya Mwakibete mkoani Mbeya, Pius Kipesha, amewataka waumini wa kanisa hilo kujitenga na dhambi, madeni na umaskini ili waweze kuishi maisha yanayompendeza Mungu na kumwabudu kwa uhuru.

Akizungumza katika ibada iliyofanyika Novemba Mosi, 2026 Mchungaji Kipesha amesema kuwa waumini wanapaswa kujitenga na mambo yanayoweza kuwazuia kuingia katika uwepo wa Mungu wakiwa katika hali nzuri ya kiroho.

Amesema kuwa adui mkubwa wa mwanadamu ni shetani na wa pili ni umaskini, hivyo amewataka waumini kuuchukia umaskini kama wanavyomchukia shetani.

Aidha, amesema kuwa kuna roho nyingine ambazo mtu asipozichukia na kujitenga nazo unaweza kukaa nazo kwa muda mrefu na kukufanya ushindwe kumwabudu Mungu kwa viwango vinavyostahili, ikiwemo kushindwa kumtolea Mungu ipasavyo.

Ameongeza kuwa Mkristo au muumini anatakiwa kuchukia shetani, dhambi na madeni ili kuishi maisha ya uhuru. 

Pia, amewatahadharisha waumini kuhusu kujenga urafiki na watu wenye tabia ya kuishi kwa madeni, akieleza kuwa tabia hizo zinaweza kuwaathiri.


Akifafanua kuhusu suala la madeni, Mchungaji Kipesha amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikopa hadi mavazi na kutoa ahadi za kulipa baadaye, jambo ambalo linaweza kuathiri maisha yao ya kiroho.

"Jitenge na madeni mtu unakopa hadi nguo, unadai wiki ijayo nitakulipa hayo mambo tukija nayo kanisani hatutaabudu ipasavyo wala kumwabudu Mungu katika roho," amesema Mchungaji Kipesha.


Aidha amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakikosana na ndugu zao pamoja na marafiki kutokana na masuala ya madeni, akiwataka waumini kubadilika, kumcha Mungu na kujiepusha na shetani ili waweze kupata matokeo mema katika maisha yao.

Hata hivyo amesisitiza kuwa watu wa Mungu wanapaswa kuwa chachu ya kuleta amani katika jamii na kuimarisha maisha yao ya kiroho.

PROFESSOR MGOKO EP 07

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment

Previous Post Next Post