" RAIS SAMIA AMKABIDHI PROF. SHEMDOE MPANGO WA TAIFA WA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI, MAMA, MTOTO, LISHE

RAIS SAMIA AMKABIDHI PROF. SHEMDOE MPANGO WA TAIFA WA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI, MAMA, MTOTO, LISHE



Na. OWM – TAMISEMI, Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, Mpango wa Taifa wa Huduma za Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto Mchanga, Mtoto na Kijana, pamoja na Lishe (2026–2030) pamoja na Taarifa ya Makadirio ya Vifo vya Kina Mama, Watoto Wachanga, Watoto Walio Chini ya Mwaka Mmoja na Watoto Walio Chini ya Miaka Mitano nchini Tanzania (2026).

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemkabidhi nyaraka hizo Prof. Shemdoe kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wake katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, mara baada ya Mhe. Rais kufungua Mkutano wa Tatu wa Kitaifa wa Kisayansi kuhusu Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana, uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, leo tarehe 26 Novemba 2026.

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewakabidhi pia nyaraka hizo kwa Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui kwa ajili ya usimamizi wa utekelezaji wake.

Sanjali na hilo, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesaini mkataba na Wakuu wa Mikoa wa Usimamizi na Utekelezaji wa Mkakati wa Kusimamia Huduma za Afya ya Uzazi, Mama, Mtoto na Vijana wa mwaka 2026/30, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wamewakilishwa na Mwenyekiti wao, Mhe. Martine Shigela, ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara.  

PROFESSOR MGOKO EPISODE 08

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post